Ijumaa , 15th Oct , 2021

Watu wenye hasira kali wamemuua muuaji aliyekiri kuwaua watoto zaidi ya 10 nchini Kenya, Masten Wanjala, ambaye alitoroka kwenye kituo cha polisi cha Jogoo Jijini Nairobi siku ya Jumatano. Wanjala ameuawa leo Oktoba 15, 2021, alfajiri majira ya saa 12:45.

Masten Wanjala, Muuaji aliyekiri kuuwa watoto zaidi ya 10

Polisi wanasema Masten Wanjala, alifuatwa na wanakijiji katika mji wa Bungoma na kupigwa hadi kufa

Wanjala alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai 2021, ambapo alikiri kutumia kemikali inayofanana na unga kwa wathiriwa kwa kuwalazimisha wainywe ama kuwapulizia usoni kabla ya kuwaua kwa kuwanyonga au kuwafyonza damu.