Alhamisi , 9th Sep , 2021

Aliyekuwa Rais wa Afghanistan kabla ya Taliban kuchukua nchi Ashraf Ghani, ameomba msamaha kwa wananchi wa Taifa hilo baada ya kukimbilia nchi za Falme za Kiarabu na kusema aliondoka baada ya kushawishiwa na usalama wa Ikulu kwamba iwapo angeendelea kuwepo kungehatarisha maisha ya raia.

Aliyekuwa Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani

Ghani aliondoka ghafla nchini Afghanistan wakati wanamgambo wa Taliban walipokuwa wakiendelea kuingia kwenye mji mkuu mnamo Agosti 15 mwaka huu.

"Niliondoka kwa kushawishiwa na usalama wa Ikulu, ulionishauri kuwa kuendelea kuwepo kulihatarisha kutokea kwa mapigano mitaani na katika barabara za mji kama ilivyotokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1990," ameeleza 

Aidha, Ghani ameongeza kuwa hakuwa na nia ya kuwaacha watu wake lakini ilikuwa ndio njia pekee iliyosalia.