
Mahakama ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela Mussa Hassan Ntakula (70), Mkazi wa Kijiji cha Ngalinje baada ya kupatikana na hatia ya kosa la udhalilishaji wa kingono ambapo hukumu hiyo imetolewa mbele ya Hakimu Mfawadhi wa Mahakama ya Wilaya ya Masasi, Rehema Iddi na mwendesha mashtaka Miraji Kajini.
Mtiwa hatiani alitenda kosa hilo April 08,2025 katika Kijiji cha Ngalinje baada ya kumlaghai Mhanga Mwanafunzi wa darasa la sita, 13 (jina la Shule limehifadhiwa) anayeishi naye Mtaa na Kijiji kimoja kwa kumwita nyumbani kisha kumvua nguo, kutoa sehemu zake za siri (uume) kisha kuchezesha kwenye nyeti za mtoto huyo