Jumamosi , 23rd Oct , 2021

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, limefanikiwa kumkamata mwanamke Janeth Peter (32), mkazi wa Kiwira wilayani Rungwe kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake mwenye umri wa siku tatu ndani ya shimo la choo, ambaye baadaye alikutwa akiwa amefariki dunia.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema,  mtuhumiwa huyo amekamatwa Oktoba 20, 2021 majira ya saa 1:00 usiku baada ya Polisi kufanya msako mkali katika Kata ya Kiwira na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo.

Matei amesema hadi sasa wanaendelea  kumhoji  pamoja na uchunguzi wa kitabibu kwa kushirikiana na wataalam wa afya ili kufahamu endapo alitoa mimba au ana matatizo ya kiafya sambamba na kufahamu sababu ya kufanya tukio hilo la kinyama.