Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, SACP Fortunatus Muslimu
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo SACP Fortunatus Muslimu, ikiwa ni siku chache baada ya mwanafunzi Faidhat Ibrahimu (13) mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mwenge iliyopo Kingolwira manispaa ya Morogoro kuuawa na Kaka yake huyo.
Kutokana na tukio hilo Kamanda Muslimu, amewataka wananchi mkoani humo kuhakikisha wanashirikiana na Jeshi hilo kutoa taarifa za migogoro kwenye familia ili kudhibiti vitendo vya mauaji.





