Jumatano , 5th Oct , 2022

Vyanzo vya kidiplomasia vya kikanda vimeeleza kuwa kiongozi wa mapinduzi Burkina Faso aliyechukua mamlaka mwezi Januari Paul-Henri Sandaogo Damiba alikimbilia katika nchi ya Togo Jumapili kufuatia mapinduzi yasiyokuwa na utulivu Afrika Magharibi mwaka 2022.

Paul-Henri Sandaogo Damiba, kiongozi wa mapinduzi Burkina Faso Januari

Mwanajeshi mwenzake, Kapt. Ibrahim Traore aliyempindua ametangaza kuungwa mkono na wakuu wa jeshi. 

Burkina Faso ndilo taifa lenye kiongozi mdogo zaidi Afrika baada ya mapinduzi. Mkuu mpya wa jeshi la Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traore, ndiye kiongozi mdogo zaidi barani Afrika. Alizaliwa mwaka 1988, hii inamfanya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 34 kuwa mkuu wa nchi mwenye umri mdogo zaidi barani Afrika.

Kapteni Traore anajiunga na viongozi wawili waliotwaa madaraka kwa njia ya mapinduzi - Kanali Mamady Doumbouya wa Guinea, aliyezaliwa mwaka 1981, na Kanali Assimi Goïta wa Mali, aliyezaliwa 1983.

Alikuwa miongoni mwa kundi la wanajeshi waliounga mkono mapinduzi ya Damiba ya Januari 24 dhidi ya rais aliyechaguliwa kidemokrasia Roch Marc Kabore.

Mara tu baada ya kunyakua madaraka kwa Capt Traore, vita vya maneno vilianza kati ya kikundi chake na kile cha Damiba, na kuzua hofu ya mzozo mkali wa madaraka. Kiongozi huyo mpya ameahidi kuimarisha usalama nchini Burkina Faso.