Jumanne , 14th Mar , 2023

Miezi sita baada ya Anastazia Mashaka kushuhudia mama yake akiuawa kwa kuchomwa visu 16 na baba yake hali iliyopelekea kukwama kwenye masomo yake kutokana na kukosa mtu wa kumlea, Halmashauri ya Mji Geita imechukua uamuzi wa kumlea na kumuhamisha shule ili aweze kuendelea na masomo yake.

Anastazia Mashaka, aliyeshuhudia mama yake akichomwa visu 16 na baba yake

Akiongea kwenye kogamano la wanawake lililofanyika mjini Geita, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Geita Rehema Mtawala, amesema mtoto huyo Januari alifukuzwa shule kutokana na kukosa ada hivyo serikali ikaamua kumuhamishia shule ya sekondari ya serikali ya Ihanamilo.

Kutokana na mtoto huyo kukosa mahitaji muhimu Halmashauri ya Mji kupitia Mkurugenzi Zahra Michuzi, wameamua kumchukua na kumlea binti huyo ili aepukane na changamoto za kimaisha anazozipitia tangu mama yake afariki na baba yake akiwa bado mahabusu.

Kwa upande wake mtoto huyo amewashukuru watu wote walioungana nae katika kipindi kigumu mpaka alipohamishiwa shule ya serikali.