Jumatano , 21st Jul , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kuwa baada ya madaktari nchini kufanya utafiti na kujiridhisha na chanjo kadhaa, amewataka Watanzania wanaohitaji kuchanjwa chanjo ya COVID-19 wajitokeze ili waweze kupata kinga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 21, 2021, wakati akihutubia Baraza la Eid El-Adha, lililofanyika katika msikiti wa Mtoro jijini Dar es Salaam.

"Maamuzi yalifikiwa kwamba basi tulete angalau chanjo kadhaa hapa madaktari fanyeni utafiti wa chanjo nzuri ambayo wenzetu wamechanja hawajapata madhara, ndiyo tukazipata chache za aina kama mbili tatu tu kati ya zote zinazozungumzwa, tukasema tuzilete hapa nchini anayetaka achanjwe," amesema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu ameongeza kuwa, "Watanzania chanjo ipo, anayetaka akachanje, hospitali zimeelezwa mahali zilipo nenda ili utimize haja, ni kinga pia sababu wenzetu wanachanja kama kinga".