Alhamisi , 29th Sep , 2022

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imesema kwamba asilimia 30 ya Watanzania wana tatizo la shinikizo la juu la damu na asilimia 33 wana uzito wa juu wa kupitiliza jambo linaloashiria kwamba wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo na Daktari bingwa wa Moyo katika taasisi hiyo Dkt. Tatizo Waane

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani, Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo na Daktari bingwa wa Moyo katika taasisi hiyo Dkt. Tatizo Waane, amesema idadi ya wagonjwa wa moyo inazidi kuongezeka kila siku jambo linalopekea hata jengo la JKCI kuwa finyu na 

Kwa upande wake Dkt Samweli Rweyimamu ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, amesema kuna watoto wanaopata magonjwa ya moyo kutokana na moyo kuwa na matundu huku mishipa ya damu ikiwa imeziba sambamba na uzito wa mtoto kukithiri 

Nao wananchi waliojitikeza kupima magonjwa ya moyo katika maadhimisho hayo, wameeleza namna magonjwa ya moyo yanavyowasumbua na kushauriwa na na daktari kuendelea kutumia dawa mpaka mwisho wa maisha yao.