Jumamosi , 17th Sep , 2022

Katibu mkuu wa michezo nchini Rwanda Didier Shema Maboko, amesimamishwa kazi na Rais wa  nchi hiyo    Paul Kagame.

Taarifa kutoka kwa waziri mkuu nchini humo Bw. Edouard Ngirente haikuweka wazi sababu za kusimamishwa kazi kwa kiongozi huyo ambaye amesimama kazi mara moja kuanzia jana. 

Maboko ameitumikia nafasi hiyo kwa karibia miaka mitatu sasa tangu alipochaguliwa mwezi  November 2019.Amekua akifanya kazi kadhaa kwenye sekta ya micheo nchini humo  ikiwemo mkurugenzi wa ufundi katika shirikisho la mpira  akikapu la Rwanda FERWABA. Makobo amewahi kuwa mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu.