Ijumaa , 10th Dec , 2021

Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi, amesema jeshi hilo limemfukuza kazi askari namba H.2324 PC Joseph kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi askari mwenzake Onesmo Joseph, baada ya marehemu kuchelewa kurejesha pikipiki ya mtuhumiwa aliyokuwa ameazima na ndipo wakaanza kuzozana

Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi, amesema kwamba tukio la kumfyatulia mwenzake risasi lilitokea wakati wote wawili wakiwa kwenye lindo la benki ya CRDB tawi la Ruangwa mkoani humo.

"Taarifa za awali zinaonesha kwamba marehemu alimuazima pikipiki askari mtuhumiwa, sasa alipochelewa kumrudishia kwenye ule muda waliokubaliana ugomvi kati yao uliendelea ukawafikisha hapo walipofikia," amesema Kamanda Kitinkwi.