Jumatatu , 20th Sep , 2021

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ametoa zawadi ikiwemo fedha na vyeti kwa maaskari polisi  walioshiriki katika tukio la kupambana na Hamza aliyezua taharuki karibu na zilipo ofisi za ubalozi wa Ufaransa Dar es Salaam Agosti 25 mwaka huu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 20, 2021, na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro.

"Askari hawa (Waliopambana na Hamza) miongoni mwao walikuwa ni Askari 11, ambao kwa mamlaka za kisheria za uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP amewapa zawadi ya vyeti vya ujasiri na zawadi ya pesa kwa kadri alivyoona inafaa," amesema Kamanda Muliro

Tazama video hapa chini