
Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imetoa hukumu hiyo katika kesi ya jinai namba 200 ya mwaka 2022 ilitolewa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Samuel Maweda.
Maweda anasema kitendo hicho kilichofanywa na mwanamke huyo ni cha kikatili na kimesababisha ndoto ya Helena ya kuhitimu darasa la saba kwa mwaka 2022 kushindwa kutimia.
Aidha mwendesha mashtaka wa Serikali, Shukrani Msuya aliieleza mahakama kuwa Oktoba 4, 2022 mshatakiwa alimpiga mtoto huyo na kumchoma moto mikono na kumsababishia maumivu kinyume na sheria.
Mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama imsamehe na kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana familia ya watoto watano ambao wanamtegemea na kuwa hilo ni kosa lake la kwanza.
Hakimu Maweda anasema kitendo kilichofanywa na mshtakiwa ni kinyume na sera ya nchi juu ya elimu kwa watoto wa kike.