Baba ampa Mimba mtoto wake

Ijumaa , 17th Jan , 2020

Deus Richard 40, mkazi wa Kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amempa ujauzito binti yake wa Darasa la Nne, Monika Shigela, na kumtelekeza mkewe na watoto wadogo watano na kutoweka kusikojulika na mtoto wake aliyempa mimba.

Mimba

Bi Mariam Masanja ambaye ndiye Mke aliyetelekezwa, amesema kuwa alipobaini uhusiano wa kimapenzi baina ya mwanae na Baba yake aliwaeleza viongozi wa Dini, kitendo ambacho kilimkasilisha bwana huyo na kuanza kuonesha bayana mapenzi yake na mtoto wake.

Aidha Mariam ameongeza kuwa licha ya ugumu wa maisha anaopitia kwa sasa, kutokana na kutelekezwa akiwa na watoto wadogo na pia ndani kukiwa hakuna chakula, anaiomba Serikali kumkamata mumewe na kumchukulia hatua kali za kisheria.