Alhamisi , 11th Jun , 2020

Leo Juni 11, 2020 Bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21 itawasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dkt. Philip Mpango Saa 10:00 Jioni. 

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango

Ikumbukwe kuwa tayari Wizara zote zimeshawasilisha makadirio ya bajeti za wizara hivyo leo bajeti kuu itahitimishwa na kupigiwa kura na wabunge kwaajili ya kupitishwa rasmi kwa matumizi kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Bajeti ya mwaka uliopita ilikuwa na jumla ya Trilioni 33.1.

Kwa mara ya kwanza Rais Magufuli alitangaza Baraza la Mawaziri lenye mawaziri 19 katika Wizara 18 alizoanza nazo mwaka 2015 mwezi Desemba.

Baada ya hapo alifanya mabadiliko mbalimbali kutokana na sababu tofauti ikiwemo kuwafuta kazi, vifo na kuwahamisha Wizara.

Wafahamu mawaziri ambao wamefanikiwa kubaki na kusoma bajeti za Wizara zao kwa miaka mitano yote ya serikali ya awamu tano bila kubadilishwa.

1. Dkt. Philip Mpango - Waziri wa Fedha na Mipango
2. Ummy Mwalimu - Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

3. Dkt. Hussein Mwinyi - Waziri wa Ulinzi 

4. Prof. Joyce Ndalichako - Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

5. Jenista Mhagama - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuuanayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

6. Willium Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Ikumbukwe kuwa leo ni siku ambayo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitasoma bajeti zake.