Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Barabara kupitika kwa 85% ifikapo 2025

Jumatano , 5th Oct , 2022

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff ameeleza kuwa katika Mpango Mkakati wa Pili utakaoanza mwaka 2021 hadi 2026 taasisi yake itatekeleza shughuli zake kwa kuzingatia vipaumbele ilivyoviandaa.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Jijini Dodoma, wakati akielezea utekelezaji wa shughuli za taasisi yake na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2022/23, Mhandisi Seff ametaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni kuzitunza barabara zilizo katika hali nzuri na hali ya wastani ili kulinda uwekezaji ambao tayari umeshafanyika.

Mpango mwingine ni kuondoa vikwazo kwenye mtandao wa barabara za wilaya ili ziweze kupitika misimu yote pamoja na kupandisha hadhi barabara za udongo kuwa za changarawe au lami kwa kuzingatia vipaumbele vya kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari katika majiji, manispaa na miji.

“Lengo la mpango mkakati wetu wa pili ni kuwa ifikapo 2025/26 asilimia 85 ya mtandao wa barabara za wilaya chini ya TARURA zitakuwa zinapitika kwa misimu yote na nyakati za mvua hapatakuwa na taharuki inayojitokeza sasa kwa maeneo mengi kutofikika”. Amesema Mhandisi Seff.

Amesisitiza kuwa, “Kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2026/27 lengo letu ni kuwa mtandao wa barabara za lami utaongezeka kwa km 1,450.75 ikiwa ni kutoka kilometa 2,404.90 hadi kufikia kilometa 3,855.65, barabara za changarawe zitaongezeka kilometa 73,241.57 ikiwa ni kutoka kilometa 29,116.57 hadi kilometa 102,358.14 na madaraja 3,808 yataongezeka kutoka madaraja 2,812 kufikia madaraja 6,620 ambapo fedha zitakazotumika kwenye mpango huu zinakadiriwa kuwa zaidi ya Shilingi trilioni 4.2.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi