Ijumaa , 16th Sep , 2022

Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), imekamilisha ujenzi wa barabara ya mchepuko kwa ajili ya kupitisha magari katika mteremko wa Inyala mkoani Mbeya, mahali ambapo zimekuwa zikitokea ajali mara kwa mara ikiwemo ile iliyosababisha kifo cha DED Igunga na dereva wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga na timu yake wakikagua barabara ya mchepuko katika eneo hilo

Kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo, imezindua  barabara  hiyo ambayo itasaidia kupunguza foleni na kukabiliana na ajali za mara kwa mara kwenye eneo la Inyala .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, amesema ujenzi wa barabara ya mchepuko umekamilika sasa wataanza kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria madereva wote watakaokiuka utaratibu uliotolewa na kikosi cha usalama barabarani.