Katibu mwenezi wa vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Twaha Mwaipaya
Akizungumza wakati akikabidhiwa ilani ya sera ambazo watazunguka nazo nchi nzima katika ofisi za makao makuu ya Chama hicho Mwaipaya amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha jambo hilo linatendeka ambapo pia amedai kuwa wanapambana kwa ajili ya watanzania.
Sambamba na hilo Mwaipaya amedai kuwa ameshangazwa na kitendo kilichofanywa na wanachama 19 walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu na kudai kuwa yeyote atakayebainika kufanya usaliti atatengwa na chama hicho.
''Sasa nayafurahia mateso ya kukaa gerezani kwa sababu ya watanzania na kupigania haki na kama wanaona usaliti ni njema tutawatenga na aliyezaliwa kwenye chumba cha haki hawezi kuishi kwenye dhuluma’ amesema Twaha Mwaipaya
Aidha Katibu huyo ameongeza kuwa anayafurahiya mateso hayo ya kukaa gerezani kwa sababu ya watanzania na kudai kuwa wasaliti wote watatengwa na chama hicho

