EWURA imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi wa Machi 2026 kuanzia leo, Machi 4, 2026.
Bei hizi zimepanda kutokana na ongezeko la bei za mafuta kwenye soko la dunia na gharama za usafirishaji. Mikoa yenye bei kubwa zaidi ya petroli ni Kagera (Bukoba) na Geita, ambapo petroli inafikia Sh3,114 na Sh3,064 kwa lita moja.
Jijini Dar es Salaam, bei mpya ya petroli ni Sh2,864 kwa lita moja (ongezeko la takriban Sh76 kutoka mwezi uliopita), dizeli Sh2,858 na mafuta ya taa Sh2,932, Bei hizi ni bei kikomo, hivyo vituo vya mafuta vinaweza kuuza chini kidogo lakini haziruhusiwi kuzidi.
Watumiaji wameshauriwa kuangalia bei rasmi na kudai risiti kila wanaponunua,
bei hizi zinaanza kutumika mara moja na EWURA inaendelea kufuatilia ili kuhakikisha ushindani wa haki na ulinzi wa wanunuzi.


