Ijumaa , 30th Jul , 2021

Kampuni ya vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers Limited imeungana mkono Kampeni ya Namthamini kwa kutoa mchango wa taulo za kike (pedi) utakaowawezesha watoto 55 kukaa shuleni kwa muda wa mwaka mzima bila kukumbana na adha ya kukosa taulo za kike.

Mhasibu na Mwakilishi wa Kampuni ya Vinywaji baridi ya Bonite Bottlers Ltd Conjesta Peter

Akizungumza na Eatv mara baada ya kukabidhi mchango huo katika Ofisi za East Africa Television zilizopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Bonite Bottlers Conjesta Peter amesema wameungana na kampeni ya Namthamini kwani ni wazi kuwa ukimsaidia mtoto wa kike unakuwa umesaidia taifa zima.

Pia Conjester Peter wamehamasisha kampuni nyingine nchini pamoja na watu mbalimbali kuungana na kampeni hiyo ili kumuwezesha mwanafunzi wakike aliyopo mjini na vijijini anayekumbana na changamoto ya taulo za kike awapo kwenye siku zake aweze kubaki shuleni.