Jumatatu , 12th Sep , 2022

Takribani watu 11  wanahofiwa kufa maji katika Pwani ya  Tunisia, huku wengine 12 wakiwa hawajulikani walipo baada ya boti iliyokua imewabeba wahamiaji 37 kuelekea nchini Italia kuzama jumanne iliyopita.   

 

Miili mingine mitano zaidi iligunduliwa juammosi usiku na kupelekea idadi hiyo ya watu 11 . Zaidi ya wahamiaji 1,000 wanasadikiwa kupoteza maisha mwaka huu pekee baada ya kujaribu kuvuka bahati ya   Mediterranean.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa mashirika ya umoja wa mataifa  ambapo  wahamiaji takribani  1,033 wanasemekana kufa ama kupotea  huku wengine  960  wakisemekana kutoswa kwenye maji na kufa. 

 Taarifa zinasema kuwa kuna milango 52,000 isiyo rasmi inayopitia kwenye bahari ya Mediterranean kati ya januari na August mwak huu huku wahamiaji wengi wakitokea nchini Tunisia, Misri na Bangladesh.