Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na ni mwanakamati wa kamati ya fedha katika bunge hilo Mhe. Nderakindo Kessy.
Bunge hilo pia limependekeza kuwapo na mfumo wa kisheria utakaoweza kuwabana wale wote watakao bainika kushiriki katika ubadhilifu.
Ripoti hiyo ya tano tangu kuanzishwa tena kwa bunge hilo imebainishwa katika vikao vya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo inaonesha kutokuwa na mabadiliko licha ya kuwepo kwa marekebisho zaidi ya elfu moja.
Mh. Nderakindo Kessy ni mbunge wa bunge la (EAC) na ni mwanakamati wa kamati ya fedha katika bunge hilo kutokea Tanzania na Mh. Abubakar Ogle ambaye pia ni mbunge wa bunge hilo kutoka nchini Kenya, ni miongoni mwa wabunge waliongea na waandishi wa habari kuhusu ripoti hiyo.
Miongoni mwa mambo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na swala la ajira kwa vijana wanaofanya kazi katika jumuiya kwa miaka mingi bila kuwa na ajira za kudumu kwa zaidi ya miaka 9, ikiwa ni matokeo ya baraza la mawaziri wa jumuiya kusitisha ajira mwaka 2009 .
Vikao vya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki limeingia katika wiki ya pili katika ujadili mambo mbalimbali yanayohusu umoja huja.