Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

BVR kuanza kusambwaza mikoani wiki ijayo

Jumatano , 15th Apr , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania itaanza kusambaza mashine za BVR 248 katika mikoa minne nchini Tanzania kuanzia katikati mwa wiki ijayo ili kuanza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.

BVR zikiwa tayari kwa ajili ya kuanza kusambazwa kwenye mikoani.

Mkuu wa kitengo cha Ufundi wa idara ya Daftrari/ICT wa NEC Dk Sisit Karia, amesema mikoa iliyoanza kupokea mashine hizi ni Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa na kwamba mpaka sasa wananchi wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Iringa wakae tayari kwani muda wowote watatangaziwa vituo vya kujiandikisha.

Mikoa zitakakopelekwa katika awamu ya pili ni Katavi, Mbeya, Dodoma, Singida Tabora Geita na Kigoma.

Pamoja na mshine hizo 248 Tume ya taifa ya uchaguzi imewaandaa wataalamu 248 ambao watakuwa na jukumu la kutoa elimu kwa wataalamu wengine 50 kwa kila mmoja nchi nzima kwa ajili ya kuharakisha uandikishaji kwa mfumo wa BVR.

Dk Sisit ameeleza kwamba wamefanikiwa kufanya maboresho makubwa katika mashine hizi ikiwa ni pamoja na kubadilisha upangaji wa vifaa (settings), mfumo endeshi (software) na upande wa vichapishio (printers) ambazo sasa zimetengenezewa nchini Ufaransa umeboreshwa na ni rahisi kusafishwa.

Mafunzo yaliyoendeshwa hapa Jijini Dar es Salaam yamechukua siku moja na yamezingatia sana upande wa vichapishio (printers), visoma alama za vidole (Finger Print Scanner) na kamera kutambua macho.

Ameongoza kwamba printer za sasa ni rahisi kusafishwa na hata kuweka kifaa kipya baada ya cha zamani kuharibika vimerahisishwa.

Kuhusu uchukuaji wa alama za vidole, amesema kwa sasa tatizo la mashine ya kuchukua alama za vidole wamelitatua kwa asilimia mia, kwani kwa wale ambao hawana alama za vidole mashine zimewekewa mfumo wa algorithm mpya ambao utatambua kila aina ya kidole.

Pia, kamera zimewekewa mfumo mpya wa kutambua macho mekundu na kurekebisha rangi ya macho mekundu (Red eyes) bila kukwamisha zoezi la uandikishaji.

Mtarajio ni kwamba zoezi la uandikishaji liwe limekamilika ndani ya kila siku 28 tokea kila mkoa unapopokea mashine hizi. Vile vile Dk Sisit ameishukuru serikali kwa kufanikisha upatikanaji wa vifaa, “serekali imejitahidi kuandaa upatikanaji wa mashine hizo, na usafirishaji kwa njia ya ndege kwenda nchi nzima. Kila halmashauri na mkoa utachukua angalau siku 28 kukamilisha mkoa utakapo pokea vifaa,” Dr Sisit amesema.

Mwisho amesema kwamba mashine nyingine 1,600 zitawasili wakati wowote. Serikali imetoa Dola za Kimarekani milioni 72 (Sh. bilioni 133). Kuwasili kwa mashine hizo, kunaifanya NEC kupokea mashine 2,098, huku ikisubiri mashine 5,902, ili kukamilisha 8,000 zinazotakiwa.

Alisema vifaa hivyo vinanunuliwa na serikali kupitia kampuni ya Lithotech Export ya Afrika Kusini, ambayo imeingia mkataba na NEC na inaviagiza kutoka China.

HABARI ZAIDI

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ