Alhamisi , 30th Jan , 2020

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo mishahara midogo kwa wafanyakazi na kusababisha kupunguza ari ya utendaji kazi.

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG), Charles Kichere.

CAG Kichere ameyabainisha hayo wakati akizungumza, katika mkutano wa kwanza wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, na kusema kuwa licha ya mishahara midogo kwa wafanyakazi wake lakini pia uhaba wa fedha unakwamisha mipango ya ujenzi wa ofisi za mikoa na kituo cha mafunzo Gezaulole.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mary Maganga, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa baraza hilo ameihakikishia ofisi hiyo kuwa Serikali itahakikisha inapunguza ama kuondoa kabisa changamoto zilizopo.