Jumanne , 2nd Dec , 2014

Chama Cha Mapinduzi CCM,kimewaagiza Mawaziri na watendaji wa wizara,wanaohusika na kero mbalimbali za mikoa ya Lindi na Mtwara,kutatua kero hizo ndani ya wiki mbili ,huku chama hicho kikibariki maamuzi yaliyofanywa na bunge kuhusu Escrow

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Bw. Abdulrahman Kinana.

Akitangaza maagizo hayo mjini Mtwara kwenye mkutano wa hadhara,Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Bw. Abdulrahman Kinana,amesema kero nyingi za wananchi hao zinatatulika,na kusema kuwa,kero hizi zinachangiwa na urasimu na umangimeza wa watendaji wa serikali,huku akisisitiza kutolizishwa na majibu toka kwa watendaji hao.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Bw. Nape Nnauye amesema kuwa,maamuzi yaliyofikiwa na kikao cha bunge mjini dodoma kuhusiana na Sakata la akaunti ya tegeta escrow,chama chake kimeafiki na kuitaka serikali kuchukua hatua kwa waliohusika na sakata hilo.

Awali akieleza matatizo ya wananchi wa Mtwara mjini,Mbunge wa jimbo hilo Mh, Hassenein Murji amesema kuwa, Halmashauri imechukua mashamba ya wananchi ili kupima viwanja,lakini wananchi wamekuwa wakisikitishwa na kitendo cha ofisi ya Waziri Mkuu kushindwa kutoa kibali cha malipo ya fidia kwa wananchi,huku halmashauri ikiwa tayari na fedha za malipo ya mashamba hayo.

Akihitimisha siku kumi na sita za ziara yake ya mikoa ya Lindi na Mtwara Katibu Mkuu huyo, ametoa wiki mbili kwa waziri wa uchukuzi Dkt. Harson Mwakyembe kutoa majibu ni kwa nini zao la korosho halisaifirishiwi katika Bandari ya Mtwara na huku korosho hizo kutoonyesha kupitia bandari ya jijini dar-es Salaam.