
Katibu wa NEC, itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka
Shaka ametoa kauli hiyo leo Wilayani Kilosa wakati akizindua Msimu Mpya wa Kilimo kwa ajili ya Wananchi mkoani Morogoro.
Amesema Rais Samia mara baada ya kuingia madarakani ameweka Msisitizo mkubwa kwenye Kilimo kwa kuitengea Bajeti kubwa Sekta hiyo katika Mwaka wa Fedha 2022/2023.
Aidha, amepongeza utekelezaji wa Ilini kwa vitendo kwa kutekeleza Ibara ya 74 ya Ilani ya uchaguzi ya ccm ya 2020-2025 kuhusu matumizi bora ya ardhi unaofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amesema Dhamira ya Serikali ya mkoa huo ni kuhakikisha Vijana wanamiliki ajira ya uhakika kupitia Sekta ya Kilimo.
Awali Mbunge wa Kilosa Profesa Paramagamba Kabudi ameipongeza Serikali kwa kurejesha Mashamba 14 kwenye Umiliki wa wananchi, ambayo yalishindwa kuendelezwa na Wawekezaji.