Jumatatu , 25th Oct , 2021

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka, amesema CCM inakemea vikali tabia inayoanza kujitokeza kwa baadhi ya watumishi wa umma wa kada mbalimbali ya uzembe na ufanyaji kazi wa mazoea usiowaheshimu wala kuwajali wananchi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka

Shaka amesema Rais Samia Suluhu Hassan, na serikali anayoiongoza wana maono, uthubutu, uzalendo, waumini wa nidhamu ya kazi na matokeo yenye kuchochea ustawi wa wananchi hivyo wanahitai watumishi wazalendo, wenye bidii, weledi na nidhamu ya kazi.

"Chama Cha Mapinduzi tunawataka watumishi wote wa umma nchini kuendeleza utendaji kazi wenye weledi, nidhamu na heshima kwa wananchi kwani hao ndio waajiri wa serikali iliyopo madarakani kwa kulipa kodi na kuiweka madarakani kwa kura zao," amesema Shaka.