Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHADEMA wamjibu Lawrence Masha

Jumatano , 15th Nov , 2017

Baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA wametoa maoni yao baada ya mwanachama wao Lawrence Masha kujivua uanachama na kujibu tuhuma alizozitoa zikiwa kama sababu za kujivua kwake.

Kwenye kurasa zao mbali mbali za mitandao ya kijamii Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameandika ujumbe akisema safari ya kupigania usawa na haki ni safari ndefu, kwa yeye mwanaume kushindwa kuhimili safari hiyo ni aibu kwani kuna wananwake ambao bado wanaendelea kuhimili ugumu wa safari.

“Lawrence Masha , struggle ya kupigania usawa,haki na demokrasia, ni safari ndefu na ngumu ,wavulana wengi wameendelea kushindwa vile vile wanaume na wanawake imara wanaendelea na safari,sio uamuzi mbaya uliochukua ila ni uamuzi wa aibu . Utajua baadaye na sio sasa”, ameandika Godbless Lema.

Naye Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema wanajua sababu za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja, na hata hivyo wanaheshimu mamuzi yake.

Tunaojua sababu za Masha kutoka CHADEMA zile kwenye barua yake tunajua ni danganya toto, tunajua sababu na tunaziheshimu. Kuthibitisha kuwa CHADEMA imejipanga kuingia ikulu, angalia takwimu za ushindi wa madiwani na wabunge nchini kuanzia 1995 hadi sasa. Ikulu ni suala la muda, tena si mrefu”, ameandika Joshua Nasari.

Pia Katibu Mkuu wa chama hiko Vicent Mashinji aesema Masha kuondoka CHADEMA ni haki yake kisheria, lakini ni vyema akaweka wazi ukweli wa sababu za yeye kuondoka.

Mheshimiwa Masha ana haki kisheria, namtakia heri, lakini lazima auambie umma nini hasa kilichotokea”, ameandika Mashinji.

Lawrence Masha hapo jana ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA akisema chama hiko hakina malengo ya kushika dola, kama ambavyo malengo ya vyama vya upinzani huwa.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali