
Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika.
Mnyika ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 14, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema majimbo ya Butiama, Handeni Vijijini, Kavuu, Kwimba, Kondoa Vijijini, Gairo, Morogoro Mjini, Songwe, Ludewa, Msalala, Lupa ni miongoni mwa majimbo ambayo uamuazi wake haujatolewa.
"CHADEMA imekata rufaa zaidi ya 400 za Udiwani lakini mpaka sasa ni rufaa 100 tu ambazo zimetolewa maamuzi suala ambalo linaminya demokrasia, kwa mfano jimbo la Ukerewe msimamizi wa uchaguzi ameanza kuengua wagombea wa udiwani ambao hawakuwekewa pingamizi", amesema Mnyika.
Kutokana na maamuzi hayo yaliyofanywa na msimamizi wa Jimbo la Ukerewe, CHADEMA imeiomba Tume kumchukulia hatua stahiki.