Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHADEMA yapata kigugumizi kuhusu Madiwani wake

Jumapili , 22nd Jul , 2018

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepatwa na kigugumizi kutaja sababu ya kuwavua uanachama madiwani wake watatu siku ya jana (Jumamosi, Julai 22) na kubaki wakisisitiza ni utovu wa nidhamu.

Akizungumza na www.eatv.tv, Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amewataja madiwani waliovuliwa uanachama kuwa ni Geofrey Kajigili wa Kata ya Sisimba, Newton Mwatujobe wa Kata ya Manga na Humphrey Ngalawa wa kata ya Iwambi Jijini Mbeya huku akishindwa kutaja sababu iliyopelekea maamuzi hayo kufanyika kwa kudai suala hilo lipo kwenye uchunguzi.

 "Ni kweli tumewavua uanachama Madiwani hao watatu kutokana na vitendo vyao vya utovu wa nidhamu walivyovionyesha ambavyo vinakinzana na chama chetu. Siwezi kusema nini hasa wamekifanya kwa kuwa jambo hilo kwa  sasa lipo kwenye Kamati Kuu linasubiriwa kufanyiwa maamuzi", amesema Mrema.

 Pamoja na hayo, Mrema amesema kwa sasa hawezi thibitisha jambo lolote kuhusu diwani Kajigili kudaiwa kumpigia kampeni hadharani Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, kwamba anastahili kuwa Mbunge wa Mbeya mjini mpaka pale Kamati Kuu itakapotoa maamuzi yao juu ya uchunguzi ambao wanaufanya.
 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi