Basi la mwendokasi lililopata ajali
Gari hiyo yenye namba T978 DHZ ilisababisha ajali hiyo wakati dereva wake akitoka Mnazi Mmoja kuelekea mzunguko wa DTV kutochukua tahadhari wakati anakatisha barabara kubwa ya Morogoro.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, amesema watu wanne wamelazwa na kuendelea kupata matibabu katika Hospitali Taifa Muhimbili akiwemo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ismail ni mtembea kwa miguu, Jumbe Mohamed (38) dereva wa gari ndogo T978 DHZ aina ya Toyota Avanza, Shukuru Omari (32)abiria wa gari ndogo na Saidi Hasani (43) abiria wa gari ndogo.






