Jumatano , 19th Oct , 2016

Bodi ya utalii nchini Tanzania imemkabidhi bendera Mtanzania Fred Uisso ambaye amechaguliwa kuwakilisha bara la Afrika kwenye fainali za mashindano ya upishi ya kidunia yafahamikayo kama “World Food Championships 2016”

Fred Uisso katika moja ya shughuli zake za mapishi

Uisso mwenye taaluma ya upishi, atashiriki mashindano hayo nchini Marekani mashindano ambayo yatafanyika Novemba 8 hadi 15 baada ya kufanya vizuri katika upishi wa nyama “Best Stake Chef” na kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho.

Chief Uisso anaendesha shuguli za upishi katika mgahawa wa Afrikando uliopo Kinondoni, anakuwa Mwafrika wa kwanza kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo, baada ya mashindano hayo kufanyika kwa muda wa miaka 15 mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kukabidhiwa bendera ya Taifa, Balozi huyo wa Red Gold Chief Uisso amesema walishiriki watu 3700 kote duniani na kwamba ushindani ulikuwa mkubwa lakini katika kila hatua alifanikiwa kupenya hadi kufikia fainali.

“Mtandao ndiyo umenifikisha hapa, maana nimeutumia vizuri na ninahakiki nitafanya vyema na kuiwakilisha Taifa na Tanzania kwa ujumla ambayo yatafanyika huko Alabama State nchini Marekani baada ya kushiriki kupitia mtandao mara kadhaa.