Jumanne , 15th Mar , 2016

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa marudio jumapili hii, Chama cha Wananchi (CUF), Visiwani Zanzibar, kimemtaka rais Dkt. John Magufuli kuingilia kati juu ya vyombo vya usalama vilivyopo visiwani humo.

Mkurugenzi wa Habari na uenezi wa Chama Cha Wananchi (CUF), Hamad Masoud Hamad,

Akiongea na Waandishi wa habari Jana visiwani humo Mkurugenzi wa Habari na uenezi wa Chama hicho visiwani Zanzibar, Hamad Masoud Hamad, amevishutumu vyombo vya usalama hasa visiwani Pemba na kusema kuwa vinasababisha wananchi kuyakimbia makazi yao.

Mkurugenzi huyo wa habari amesema kuwa Rais Magufuli anatakiwa kuingilia kati suala hilo kwa kuwa yeye ndio Amiri Jeshi Mkuu ambae ana jukumu la kusimamia vyombo vyote vya usalama nchini.

Hamad Masoud amesema kuwa Rais Magufuli anapasawa kukataa kuhadaiwa na wasaidizi wake kuhusu usalama wa Visiwa hivyo na kusema kuwa anatakiwa akomesha matumizi mabaya ya vyombo hivyo yanayojiri visiwani humo.