Jumatatu , 28th Sep , 2015

Ushirikiano mzuri kati ya walimu na wazazi unaweza kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi mkoani Iringa.

Jengo la Ofii ya Chama cha Walimu Mkoa wa Iringa (CWT).

Mwenyekiti wa Chama cha walimu (CWT) mkoani Iringa Bw. Stanslaus Mhogolo amewakumbusha wazazi kuwapelekea watoto wao shule ili kukuza sekta ya elimu nchini.

Mwenyekiti wa shule ya msingi Msukanzi wilayani Iringa vijijini Bw. Nothrick Mkiwa amewakumbusha wazazi kutowapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani ili kuwapa nafasi ya kusoma.

Aidha, amesema serikali itawachukulia hatua za kisheria wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto wao shule.

Hata hivyo, Bw. Mkiwa amesema elimu ni nyenzo pekee ambayo itawasaidia watanzania kuendeleza rasilimali zilizopo nchini na kuondokana na tabia ya kutegemea wawekezaji kutoka nje ya nchi.