Jumatatu , 2nd Mar , 2015

Serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) imesema kitendo cha serikali kutochukua hatua madhubuti za kukabiliana na vitendo vya mauaji ya watu wenye albinism kinachangia kuongezeka vya mauaji ya watu hao nchini.

Akiongea leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Jinsia na Makundi Maalum wa (DARUSO), Rose Makupa amesema zaidi ya matukio 120 ya kesi yameripotiwa huku kesi 11 zikiwa zimefikishwa mahakamani na kesi tano pekee zikiwa zimetolewa hukumu jambo linalohusishwa na viongozi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wanafunzi wenye albinism wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Perpetua Senkoro amesema vyombo vya sheria na usalama vimekuwa havifanyi upelelezi wa kina ili kuwatia hatiani watuhumiwa.

Tags: