
Kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi ya wateja na watumiaji wa maji ya Dawasco jijini Dar es Salaam,Mamlaka hiyo imeboresha kiwango cha ubora wa maji kutoka vyanzo vyake hadi kuwafikia watumiaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwenye maonyesho ya wiki ya maji ambayo yanahusisha nchi zaidi ya nne mtaalamu wa kitengo cha maji kutoka Dawasco bwana Siza Mongera amesema kuwa tayari ofisi hiyo inaendelea kuyafanya uchunguzi wa kina na kuyatibu maji hayo ili yawafikie watumiaji wa maji hayo yakiwa salama kwa ubora unaotakiwa.
Kwa upande wake mshiriki wa maonyesho hayo bwana Paul Mzena amewataka watanzania kuhakikisha wanatmia miundombinu bora ya usambazaji wa maji ili tozo watakazotozwa ziwe sambamba na matumizi ya huduma ya maji.
