Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Seriel Mchembe ameyasema hayo kwenye ibada maalumu ambayo imeyakutanisha makanisa yote wilayani hapa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kutokana na kupungua kwa maambukizi ya virusi vya corona.
"Kuna mwanasiasa aliniambia Tanzania kuna watu Milioni 1 watafariki, nikamwambia utaanza kufariki wewe kabla hata Sisimizi hajafariki" amesema DC Mchembe
Kwa upande wao baadhi ya waumini wamesema kuwa wataendelea kufanya kazi bila kuogopa chochote huku wakiwashangaa watu wasioitakia mema nchi ya Tanzania dhidi ya virusi vya corona.
Tazama video kamili hapo chini