Jumatano , 19th Dec , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema demokrasia kwa sasa imehamia Bungeni kuwa hivyo wabunge mbalimbali watumie jukwaa hilo kueleza madai yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye Uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya njia 8 kutoka Kimara hadi Kibaha yenye urefu wa kilomita 19.

Rais Magufuli amesema, "aliposimama hapa kazungumzia Demokrasia, sijui demokrasia gani anataka, tumekaa hapa CCM, CHADEMA na CUF, ameitwa kwenye mkutano ambao Rais ni Mwenyekiti wa CCM anazungumza, sijui anataka demokrasia gani, demoktasia sio fujo"

"Tungekuwa wabaya sisi CCM, tusingeweka hii barabara Dar, kwa sababau hata Mstahiki Meya sio wa CCM ila namshukuru maana anajua kabisa huku ndio kutekeleza ilani ya CCM."

Awali akizungumza kwenye Mkutano huo, Mbunge wa jimbo la Kibamba, John Mnyika alimuomba Rais Magufuli kuboresha suala la demokrasia nchini na kubainisha kuwa ana ujumbe kutoka kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.