Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt Charles Msonde
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa hii leo Mei 11, 2022, ambapo pia Rais Samia amemteua Dkt. Maduhu Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, kabla ya uteuzi huo Dkt. Kazi alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania.
Mbali na uteuzi huo pia, Rais Samia amefanya uhamisho kwa Manaibu Makatibu Wakuu, ambapo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Ramadhan Kombweyi, amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na kuchukua nafasi ya Dkt. Switbert Mkama, ambaye amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kuwa Naibu Katibu Mkuu.