Jumanne , 6th Dec , 2022

Kamati Kuu ya CCM imempendekeza mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kugombea tena nafasi ya ueyekiti kwa kipindi cha miaka 5 ijayo pamoja na Makamu Mwenyekiti anayemaliza muda wake Ndugu Abdulrahman Kinana kugombea tena miaka 5

Viongozi hao kesho watapigiwa kura na wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa

Aidha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Shaka Hamdu Shaka amesema kwa mara ya kwanza wagombea wengi wamejitokeza kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya CCM 
Jumla ya wajumbe wanaohitajika ni 30 (15 Bara na 15 Zanzibar) lakini waliojitokeza kugombea nafasi hizo ni wanachama 2703