Ijumaa , 21st Feb , 2020

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, amesema kuwa watu wanaoishi visiwani wanakumbwa na changamoto ya usafiri wa majini, kwani kwa kiasi kikubwa hugharimu maisha yao, pindi unapotokea upepo mkali ama Tsunami.

Meli ya Mv Spice Islanders iliyozama mwaka 2011.

Dkt Shein ameyabainisha hayo leo Februari 21, 2020, katika Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Masuala ya Maafa katika Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na ndipo alipolikumbuka tukio lililoleta simanzi kwa watu wengi visiwani humo la kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islanders.

"Waliokuwapo hapa wanakumbuka uzuri ajali iliyoacha athari isiyosahaulika ya Meli maarufu ya Spice Islanders katika eneo la Nungwi na ilikuwa na watu wengi ambao idadi yake haijulikani mpaka leo, inakisiwa waliozama ni zaidi ya 700, waliokolewa ni zaidi ya watu 600 na hatujui wengine wamepotelea wapi na ilipozama ni Bahari yenye kina kikubwa" amesema Rais Shein.

Meli ya Mv Spice Islander, ilizama Septemba 9, 2011, katika eneo la Nungwi,  wakati ikitokea Unguja kuelekea Pemba.