Alhamisi , 28th Dec , 2017

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani  nchini (SACP) Fortunatus Muslim ametoa tathmini ya ajali zilizotokea siku ya Krismasi na kutaja kuwa zimepungua ukilinganisha na mwaka jana.

Akiongea na waandishi wa habari  leo Jijini Dar es Salaam Kamanda Muslim amesema kuwa siku ya Krismasi mwaka huu ajali zilizotokea zimesababisha nusu tu ya vifo vilivyotokea mwaka jana.

“Disemba 25 siku ya Krismasi zilitokea ajali 10 tu nchi nzima  na kusababisha vifo 5 na majeruhi 11, ukilinganisha na mwaka jana ambapo zilitokea ajali 14 na kusababisha vifo 10 na majeruhi 15”, amesema Kamanda Muslim.

Aidha kamanda Muslim amewataka madereva kuendelea kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha sikukuu  na kuzingatia sheria za barabarani.