Jumatatu , 19th Sep , 2022

Familia ya mtoto Bennet Kiwelu, mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Mt. Sayuni, Dar es Salaam, aliyefariki dunia kwa madai ya kushambuliwa shuleni na mwalimu, imesema kuwa habari hizo siyo za kweli, bali alifariki kutokana na tatizo lake la kiafya na si kutokana na adhabu shuleni.

Mtoto Bennet Kiwelu

Dkt. August Mtui ambaye ni mjomba wa marehemu amesema kwa mujibu wa historia ya afya ya marehemu na ripoti za kitabibu, zinaashiria kwamba Bennet alikuwa na tatizo la kiafya ambalo limepelekea kifo chake baada ya kuzimia akiwa shuleni na baadaye kupoteza maisha Alfajiri Septemba 18 katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa zaidi usikose kutazama EATV SAA 1, ifikapo saa 1:00 jioni ndani ya East Africa TV.