Alhamisi , 16th Sep , 2021

Katika kuimarisha na kuboresha Ulinzi wa Wanyamapori aina ya Faru nchini  dhidi ya vitendo vya ujangiri, Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori nchini TAWA, imeanza zoezi la kuwafunga Vifaa maalumu vya mawasiliano Faru wote waliopo katika pori la akiba Maswa,ili kufuatilia nyendo zao.

Mmoja wa Faru akifungwa kifaa hicho

Vifaa hivyo vinafungwa kwa kushirikiana na shirika la uhifadhi la Ujerumani la Frunk Furt Zoological Society, lengo ikiwa ni kufuatilia nyendo zao pamoja na kupata taarifa nyeti dhidi ya uhifadhi wa wanyama hao,ambao wapo katika orodha ya wanyamapori walio katika tishio la kutoweka.

Tazama Video hapo chini