Mwezi Julai mamlaka za nchi hiyo zilitnagaza uwepo wa ugonjwa huo hatari ambao unaambukizwa , ukiwa na dalili kama za Ebola ,baadz ya kutokea vifo viwili ambayo vilihusishwa na ugonjwa huo. Lakini uchunguzi wa baadae ulibaini kwamba vifo hivyo vilisababishwa na matatizo mengine
Watu watatu ambao walikutwa na virusi hivyo akiwemo mtoto mwenye umri wa miezi 14 walikua chini ya uangalizi maalum ambapo baadae walionekana kuendelea vyema na afya zao.
Watu 200 ambao walikua na ukaribu na watu hao ,pia walifuatiliwa kwa ukaribu na kuja kugundulika kwamba hawana mamabukizi yoyote.

