Jumapili , 30th Oct , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba serikali yake inaendelea na ujenzi pamoja na utanuzi wa viwanja vya ndege na kwamba hakuna kiwanja kilichosimama ujenzi wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 30, 2022, wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Msalato jijini Dodoma.

"Kwa mwaka huu wa fedha tumepanga kuanza ujenzi na utanuzi wa viwanja vya Tabora, Shinyanga, Kigoma na Sumbawanga, tunasubiri watoaji fedha waseme hawana mashaka na miradi hii ili fedha ipatikane tuvijenge, kazi ya ujenzi na kukuza usafiri wa anga inaendelea na hakuna kiwanja kilichosimama ujenzi wake," amesema Rais Samia.

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa, "Mradi huu unatoa fursa za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa wananchi wanaozunguka eneo hili, wasimamizi wa miradi hakikisheni kazi zinazostahili kufanywa na Watanzania zifanywe na watanzania,"