
Alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika makazi ya Maale Adumim yaliyoko katika Ukanda wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Netanyahu alisaini rasmi hati ya kuidhinisha ujenzi wa maelfu ya nyumba mpya karibu na eneo hilo, kama sehemu ya mpango tata wa kupanua makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika Ukanda wa Magharibi. Mpango huo unatarajiwa kukata kabisa muunganisho kati ya Ukanda wa Magharibi na Jerusalem ya Mashariki.
Mradi huo uliidhinishwa mwezi uliopita na serikali ya mrengo wa kulia ya Israel. Serikali kadhaa za Magharibi, zikiwemo Ujerumani na Ufaransa, zimeukosoa vikali mpango huo.
Makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika Ukanda wa Magharibi, ambao Israel iliukalia mwaka 1967, ni kinyume cha sheria za kimataifa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki.