
Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 8, 2022, Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia kwenye taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Maendeleo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali kwa mwaka wa 2023/2024 pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
"Sasa hivi GDP per capital yetu inakadiriwa mwishoni mwa mwaka itakuwa dola 990 tumerudi chini tutaenda kwenye kundi la nchi maskini kufuatana na viwango vilivyowekwa na Benki ya Dunia, tusiongelee uchumi wa kati hatuko huko tena, tumeshuka," amesema Profesa Muhongo