Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Nape Nnauye
Mhe. Nape ameyasema hayo Mkoani Morogoro kwenye kikao cha kazi cha mameneja na maafisa uhusiano wa serikali ambapo amesema malalamiko makubwa ya waandishi wa habari ni kukosa ushirikiano baina yao na maafisa hao na kwamba hali hiyo inasababisha wandishi wa habari kuiandika vibaya serikali na taasisi zake.
Waziri huyo ameongeza kwa kuwataka maafisa hao kuacha mara moja tabia hiyo kwani wanawanyima wananchi haki ya kupata tarifa za utendaji kazi wa serikali na hivyo kuona serikali haijafanya lolote katika kuleta maendeleo.
Katibu mkuu wa wizara hiyo Pro. Elisante Ole Gabriel katika kikao hicho amemuomba waziri kutatua changamoto za maafisa hao zikiwemo kuongeza bajeti ili wapate vitendea kazi vya kutosha na kuongeza ufanisi katika kazi.
Kwa upande wao baadhi ya maafisa uhusiano wamekiri kuwepo changamoto ya maafisa kuwakimbia waandishi wa habari ambapo wamesema kutokana na mafunzo pamoja na ushauri walioupata watahakikisha wanarejesha ushirikiano huo





