Haya ndio Majimbo ya uchaguzi yaliyofutwa

Alhamisi , 2nd Jul , 2020

Tume ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza kufuta majimbo manne 4 ya uchaguzi kutokana na changamoto tofauti ikiwemo ongezeko la idadi ya watu katika maeneyo mbalimbali ya mjini na vijijini.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid amesema Tume imezijadili changamoto katika maeneo husika na kujiridhisha ndipo ikaamua kuyafuta majimbo hayo kutokana na mamlakla iliyopewa kupitia kifungu cha 120 (4) cha katiba ya Zanzibar.

Aidha amesema ni kosa kwamtu yoyote kutoa tamko kabla ya tume kutangaza siku ya uchaguzi kwani kufanya hivyo ni kuingilia kazi ya Tume na hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Thabit Idarous Faina amewaomba wazanzibar kutokua na hofu ya upatikananji wa vitambulisho vya kupigia kura kwani utaratibu unaendelea na kupatiwa mara tu tume itakapokamilisha utaratibu wake.
 

Tazama Video hapo chini yakitajwa majimbo